Usiku Wa Valentine (the Night Of Valentine)

CHAPTER ONE

"Nothing last forever,live the moment"

Ni miaka mitatu sasa imetimia tangu mimi na kelvin tuanze mahusiano yetu.Tuliwekeana mipango mingi pamoja ya kuwa pamoja siku zote,kusaidiana na kupendana daima.Nyumbani kwetu hawakujua kama nipo kwenye mahusiano yoyote yale na mara nyingi mama yangu alikua akikaa na mimi kuniuliza,.Naitwa Janeth Damian..songa na mimi kwenye mkasa ulionikuta ndani ya ujana wangu,
Nikiwa na Mama tumekaa tunakula chakula cha mchana, alianza kuniuliza maswali
Mama;Enhe Janeth utaniletea mkwe lini?
Janeth;Aaah mama,mkwe gani tena
Mama;Mhh ina maana umesoma kote huko bado hutaki nionesha mkwe wangu
Janeth;Mama bhana (huku nikicheka)
Mama;Aya we mfiche siku likikutokea puani ,ntakupa kitambaa
Tuliongea mambo mengi na mama ,story nyingi ..baada ya kumaliza kula nilivitoa vyombo na kwenda kuosha..Mtu yoyote ambaye alikua karibu nami aliamini kuwa mimi bado ni binti sina mchumba..Vijana wengi wa mtaani walinitongoza na kutaka kuwa pamoja nami lakini hakuna niliyemkubali wala kuvutiwa nae..Kelvin wangu ndo mwanaume ninayempenda sana ,urefu wake,mwili wake,ukarimu wake kwangu na yote aliyokuwa akinionesha mapenzi moto moto bila kuona aibu yoyote hata mbele ya marafiki zangu.,Kwangu ilikua ni furaha tu kwani,nilitaman sana mwanaume aniweke wazi mbele ya kila mtu anayetuona …...Marafiki nlikua nao wengi lakini sikupenda kuamini mtu yoyote kwenye swala la mahusiano,Kelvin alikua akinionesha upendo wote kwa dhati,Tumesoma wote Chuo kikuu cha Dar es Salaam ,kozi tofauti tofauti lakini mda wa kukutana hatukukosa kabisa.,siku moja wakati tumekutana maongezi yetu yalikua hivi:

Kelvin;mambo J

Janeth;Poa,mzima love

Kelvin;mzima mpenzi wangu,sijui wewe

Janeth;mzima pia
Kelvin;Nakupenda sana Janeth wangu,urembo wako ni kama ua lichanualo asubuhi na kung’aa,upole wako ni kama nuru iangazayo angani,,You mean a world to me,never will I think of giving up on you,You are my love ,I adore you,
Janeth;Mhhh babe
Kelvin;Yah surely,I promiseYnah

Edited: 02.03.2021

Add to Library


Complain